Swali: Nilimuuliza mama yangu kuhusu baba yangu ambaye akasema kwamba alikuwa anafanya kheri, lakini hakuwa akiswali. Je, inajuzu kwangu kuhiji kwa niaba yake, kumuombea msamaha na kumuombea du´aa?
Jibu: Ikiwa hakuwa akiswali basi yeye ni kafiri. Katika hali hiyo hahijiwi wala kuombewa du´aa. Allaah (Jalla wa ´Alaa) amesema:
مَا كَانَ لِلنَّبِيِّ وَالَّذِينَ آمَنُوا أَن يَسْتَغْفِرُوا لِلْمُشْرِكِينَ وَلَوْ كَانُوا أُولِي قُرْبَىٰ مِن بَعْدِ مَا تَبَيَّنَ لَهُمْ أَنَّهُمْ أَصْحَابُ الْجَحِيمِ وَمَا كَانَ اسْتِغْفَارُ إِبْرَاهِيمَ لِأَبِيهِ إِلَّا عَن مَّوْعِدَةٍ وَعَدَهَا إِيَّاهُ فَلَمَّا تَبَيَّنَ لَهُ أَنَّهُ عَدُوٌّ لِّلَّـهِ تَبَرَّأَ مِنْهُ ۚ إِنَّ إِبْرَاهِيمَ لَأَوَّاهٌ حَلِيمٌ
“Haimpasi Nabii na wale walioamini kuwaombea maghfirah washirikina, japokuwa ni jamaa zao wa karibu, baada ya kuwabainikia kwamba wao ni watu wa Motoni. Hayakuwa maombi ya Ibraahiym kumuombea baba yake isipokuwa kwa sababu ya ahadi aliyoahidiana naye, lakini ilipombainikia kwamba yeye ni adui wa Allaah alijiepusha naye. Hakika Ibraahiym [alikuwa] ni mwenye huruma mno na mvumilivu.”[1]
Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:
”Baina ya mtu na kufuru na shirki ni kuacha swalah.”
”Ahadi iliyo baina yetu sisi na wao ni swalah. Hivyo basi yeyote atakayeiacha amekufuru.”
Swalah ni nguzo ya Uislamu. Mwenye kuilinda ameilinda dini yake na mwenye kuipuuza ameipoteza dini yake.
[1] 09:113-114
- Muhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
- Tarjama: Firqatunnajia.com
- Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/30939/هل-يجوز-الاستغفار-لميت-كان-لا-يصلي
- Imechapishwa: 13/09/2025
Swali: Nilimuuliza mama yangu kuhusu baba yangu ambaye akasema kwamba alikuwa anafanya kheri, lakini hakuwa akiswali. Je, inajuzu kwangu kuhiji kwa niaba yake, kumuombea msamaha na kumuombea du´aa?
Jibu: Ikiwa hakuwa akiswali basi yeye ni kafiri. Katika hali hiyo hahijiwi wala kuombewa du´aa. Allaah (Jalla wa ´Alaa) amesema:
مَا كَانَ لِلنَّبِيِّ وَالَّذِينَ آمَنُوا أَن يَسْتَغْفِرُوا لِلْمُشْرِكِينَ وَلَوْ كَانُوا أُولِي قُرْبَىٰ مِن بَعْدِ مَا تَبَيَّنَ لَهُمْ أَنَّهُمْ أَصْحَابُ الْجَحِيمِ وَمَا كَانَ اسْتِغْفَارُ إِبْرَاهِيمَ لِأَبِيهِ إِلَّا عَن مَّوْعِدَةٍ وَعَدَهَا إِيَّاهُ فَلَمَّا تَبَيَّنَ لَهُ أَنَّهُ عَدُوٌّ لِّلَّـهِ تَبَرَّأَ مِنْهُ ۚ إِنَّ إِبْرَاهِيمَ لَأَوَّاهٌ حَلِيمٌ
“Haimpasi Nabii na wale walioamini kuwaombea maghfirah washirikina, japokuwa ni jamaa zao wa karibu, baada ya kuwabainikia kwamba wao ni watu wa Motoni. Hayakuwa maombi ya Ibraahiym kumuombea baba yake isipokuwa kwa sababu ya ahadi aliyoahidiana naye, lakini ilipombainikia kwamba yeye ni adui wa Allaah alijiepusha naye. Hakika Ibraahiym [alikuwa] ni mwenye huruma mno na mvumilivu.”[1]
Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:
”Baina ya mtu na kufuru na shirki ni kuacha swalah.”
”Ahadi iliyo baina yetu sisi na wao ni swalah. Hivyo basi yeyote atakayeiacha amekufuru.”
Swalah ni nguzo ya Uislamu. Mwenye kuilinda ameilinda dini yake na mwenye kuipuuza ameipoteza dini yake.
[1] 09:113-114
Muhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
Tarjama: Firqatunnajia.com
Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/30939/هل-يجوز-الاستغفار-لميت-كان-لا-يصلي
Imechapishwa: 13/09/2025
https://firqatunnajia.com/duaa-kwa-baba-ambaye-alikuwa-haswali/