Du´aa inayosemwa wakati adhaana ikiendelea

Swali: Ni lini mtu anatakiwa kusoma du´aa isemayo:

وأنا أشهدُ أن لا إلَهَ إلَّا اللَّهُ وحدَهُ لا شريكَ لَهُ و أنَّ محمَّدًا عبدُهُ ورسولُهُ رضيتُ باللَّهِ ربًّا وبالإسلامِ دينًا وبمحمَّدٍ رسولا

“Na mimi nashuhudia ya kwamba hapana mungu wa haki isipokuwa Allaah, hali ya kuwa yupekee hana mshirika, na kwamba Muhammad ni mja na Mtume Wake.”?

Jibu: Udhahiri wa Hadiyth ni kwamba pale muadhini anaposema:

أَشْهَدُ أَنْ لا إِله إِلا الله أَشْهَدُ أَنْ لا إِله إِلا الله أَشْهَدُ أَنَّ مُحَمَّداً رَسُولُ الله أَشْهَدُ أَنَّ مُحَمَّداً رَسُولُ الله

“Nashuhudia ya kwamba hapana mungu wa haki isipokuwa Allaah. Nashuhudia ya kwamba hapana mungu wa haki isipokuwa Allaah. Nashuhudia ya kwamba Muhammad ni mja na Mtume Wake. Nashuhudia ya kwamba Muhammad ni mja na Mtume Wake.”

Nawe utatakiwa urudilie hivo, kisha baada ya hapo useme:

رضيتُ باللَّهِ ربًّا وبالإسلامِ دينًا وبمحمَّدٍ رسولا

“Naridhia Allaah kuwa ndiye Mola, Uislamu ndio dini na Muhammad (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) ndiye Mtume.”

Imekuja katika tamko jengine:

“Anayesema wakati anaposikia muadhini:

وأنا أشهدُ أن لا إلَهَ إلَّا اللَّهُ وحدَهُ لا شريكَ لَهُ و أنَّ محمَّدًا عبدُهُ ورسولُهُ رضيتُ باللَّهِ ربًّا وبالإسلامِ دينًا وبمحمَّدٍ رسولا

“Na mimi nashuhudia ya kwamba hapana mungu wa haki isipokuwa Allaah, hali ya kuwa yupekee hana mshirika, na kwamba Muhammad ni mja na Mtume Wake. Nimeridhia Allaah kuwa Mola, Uislamu kuwa ndio dini na Muhammad kuwa Mtume.”

basi Allaah atamsamehe madhambi yake.”

Sentesi isemayo “Nami nashuhudia… “ inafahamisha kuwa mtu anatakiwa kusema hivo baada ya maneno ya muadhini.

  • Muhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Tarjama: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Majmuu´-ul-Fataawaa (12/194-195)
  • Imechapishwa: 12/08/2026