Swali: Kundi la watu hawajui wakati wa alfajiri na wanaswali kwa kutegemea taarifa ya mtu wanayemwamini. Hata hivyo baadhi yao wana mashaka.
Jibu: Muda wa kuwa wanawaamini na wanajua kuwa bwana huyo ana utambuzi wa wakati wa kuingia alfajiri, basi hapana shaka kinachowalazimu. Kwa sababu haijawabainikia kuwa wameswali kabla ya wakati. Kwa msemo mwingine hakuna neno kwao. Lakini midhali wako na mashaka, basi wanatakiwa kuchukua tahadhari na wasiswali mpaka watapokuwa na dhana yenye nguvu au yakini kuwa kumeshapambazuka. Hilo ni jambo ambalo kuzinduliwa nalo na waambiwe wasubiri dakika 5-10 baada ya kuingia alfajiri. Hilo haliwadhuru. Ni bora kuswali kwa dakika 10-15 kwa kuchelewa kuliko kuswali mapema kwa dakika 1 kabla ya kuingia wakati.
- Muhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
- Tarjama: Firqatunnajia.com
- Marejeo: Majmuu´-ul-Fataawaa (12/215)
- Imechapishwa: 12/08/2026
Swali: Kundi la watu hawajui wakati wa alfajiri na wanaswali kwa kutegemea taarifa ya mtu wanayemwamini. Hata hivyo baadhi yao wana mashaka.
Jibu: Muda wa kuwa wanawaamini na wanajua kuwa bwana huyo ana utambuzi wa wakati wa kuingia alfajiri, basi hapana shaka kinachowalazimu. Kwa sababu haijawabainikia kuwa wameswali kabla ya wakati. Kwa msemo mwingine hakuna neno kwao. Lakini midhali wako na mashaka, basi wanatakiwa kuchukua tahadhari na wasiswali mpaka watapokuwa na dhana yenye nguvu au yakini kuwa kumeshapambazuka. Hilo ni jambo ambalo kuzinduliwa nalo na waambiwe wasubiri dakika 5-10 baada ya kuingia alfajiri. Hilo haliwadhuru. Ni bora kuswali kwa dakika 10-15 kwa kuchelewa kuliko kuswali mapema kwa dakika 1 kabla ya kuingia wakati.
Muhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
Tarjama: Firqatunnajia.com
Marejeo: Majmuu´-ul-Fataawaa (12/215)
Imechapishwa: 12/08/2026
https://firqatunnajia.com/hawajui-wakati-wa-swalah-na-wanaswali-kwa-kutegemea-taarifa-ya-mtu-mwaminifu/