Swali: Mtu aseme nini baada ya Rukuu´ pale anapokuwa amesimama kunyooka sawasawa?
Jibu: Aseme:
رَبَّنَا وَلَكَ الْحَمْدُ، حَمْداً كَثيراً طَيِّباً مُبارَكاً فِيهِ أَهلَ الثَّناءِ وَالْمَجْدِ، أَحَقُّ مَا قَالَ الْعَبْدُ، وَكُلُّنَا لَكَ عَبْدٌ. اللَّهُمَّ لاَ مَانِعَ لِمَاأَعْطَيْتَ، وَلاَ مُعْطِيَ لِمَا مَنَعْتَ، وَلاَ يَنْفَعُ ذَا الجَدِّ مِنْكَ الجَدُّ
“Ee Mola wetu, sifa zote njema ni Zako, sifa nyingi, nzuri na zilizobarikiwa ndani yake. Wewe ni mstahiki wa sifa na utukufu, ni ukweli yale yaliyosemwa na mja, na sisi wote Kwako ni waja. Ee Allaah! Hapana awezaye kukizuia kile Ulichokitoa na hapana awezaye kukitoa kile Ulichokizuia na wala haumnufaishi mwenye utajiri, kwani Kwako Wewe ndiko kunatoka utajiri.”[1]
Akariri himdi na sifa. Baina ya Sujuud mbili aseme:
رب اغفر لي، رب اغفر لي
“Ee Mola! Nisamehe! Ee Mola! Nisamehe!”
Akariri:
اللهم اغفر وارحمني واهدني واجبرني وارزقني
“Ee Allaah! Nisamehe, unirehemu, uniongoze, uniunge na uniruzuku.”
اللهم اغفر لي وارحمني، اللهم أصلح قلبي وعملي، اللهم اغفر لي ولوالدي
“Ee Allaah! Nisamehe na unirehemu. Ee Allaah! Utengeneze moyo wangu. Ee Allaah! Nisemehe mimi na wazazi wangu.”
Akariri du´aa.
[1] Muslim (477).
- Muhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
- Tarjama: Firqatunnajia.com
- Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/22630/ما-يقال-في-الرفع-من-الركوع-وبين-السجدتين
- Imechapishwa: 14/07/2023
Mshirikishe mwenzako:
- Click to share on Telegram (Opens in new window) Telegram
- Click to share on WhatsApp (Opens in new window) WhatsApp
- Click to print (Opens in new window) Print
- Click to email a link to a friend (Opens in new window) Email
- Click to share on Facebook (Opens in new window) Facebook
- Click to share on X (Opens in new window) X
- Click to share on Pocket (Opens in new window) Pocket
Related
18. Du´aa za kuinuka kutoka kwenye Rukuu´
38- سَمِعَ اللَّهُ لِمَنْ حَمِدَهُ "Allaah amemsikia mwenye kumhimidi."[1] 39- رَبَّنَا وَلَكَ الْحَمْدُ، حَمْداً كَثيراً طَيِّباً مُبارَكاً فِيهِ "Ee Mola wetu, sifa zote njema ni Zako, sifa nyingi, nzuri na zilizobarikiwa ndani yake."[2] 40- ربَّنا ولك الحمدُ مِلْءَ السَّمواتِ ومِلْءَ الأرضِ ومِلْءَ ما شِئْتَ مِن شيءٍ بعدُ أهلَ الثَّناءِ والمجدِ…
In "Huswn-ul-Muslim"
14. Du´aa katika Rukuu´, baada ya Rukuu´, katika Sujuud na baina ya Sujuud mbili
68- Hudhayfah (Radhiya Allaahu ´anhu) amesema kuwa amemsikia Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) akisema katika Rukuu´: سبحان ربي العظيم “Ametakasika Mola Wangu, aliye Mtukufu.” Alisema hivo mara tatu. Anapoenda katika Sujuud akisema: سبحان ربي الأعلى “Ametakasika Mola Wangu, Aliye juu.” Alisema hivo mara tatu. 69- ´Aliy (Radhiya Allaahu ´anhu)…
In "Swahiyh-ul-Kalim at-Twayyib"
52. Kuinuka kutoka katika Rukuu´ na du´aa zake
Baada ya hapo alikuwa (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) akiuinua mgongo wake kutoka katika Rukuu´ na kusema: سَمِعَ اللهُ لِمَنْ حَمِدَه “Allaah amemsikia mwenye kumhimidi.”[1] Vivyo hivyo alimwamrisha yule mtu aliyeswali vibaya na kumwambia: “Haitimii swalah ya yeyote mpaka... alete Takbiyr... aende katika Rukuu´... halafu aseme: سَمِعَ اللهُ لِمَنْ حَمِدَه…
In "Swifatu Swalaat-in-Nabiy"