Swali: Unasemaje juu ya wale wanaoigawa Sunnah katika Sunnah inayotambulika na Sunnah isiyotambulika na matokeo yake wanawavuta vijana kutozifanyia kazi zile Sunnah ambazo watu hawazitambui na ambazo ni ngeni kwa wengine? Hoja yao eti ni kutowakimbiza watu mbali na dini na ulingano.
Jibu: Wanachotaka ni dini kufuata matamanio. Hivyo tunapoenda kwa mabedui ambao hawajui chochote katika Sunnah za Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam), maana yake ni kwamba nasi tuziache Sunnah? Na tunapokuwa kati ya wanazuoni lakini ambao wanachukulia wepesi, tuziache? Matokeo yake dini inakuwa ni mchezo. ´Aliy (Radhiya Allaahu ´anh) amesema:
“Waelezeni watu kwa wanayoyajua. Je, mnataka akadhibishwe Allaah na Mtume Wake (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam)?”
Muslim amepokea kwa cheni ya wapokezi iliokatika katika utangulizi wa “as-Swahiyh” yake kwamba Ibn Mas´uud (Radhiya Allaahu ´anh) amesema:
“Hutowaeleza watu jambo ambalo halifahamiki na akili zao, isipokuwa litakuwa ni fitina kwa baadhi yao.”
Tunawalingania watu na kuwafunza. Tunaanza kuwafundisha kwa maneno na kwa vitendo.
- Muhusika: ´Allaamah Muqbil bin Haadiy al-Waadi´iy
- Tarjama: Firqatunnajia.com
- Marejeo: Qam´-ul-Mu´aanid, uk. 401-402
- Imechapishwa: 08/07/2025
Mshirikishe mwenzako:
- Click to share on Telegram (Opens in new window) Telegram
- Click to share on WhatsApp (Opens in new window) WhatsApp
- Click to print (Opens in new window) Print
- Click to email a link to a friend (Opens in new window) Email
- Click to share on Facebook (Opens in new window) Facebook
- Click to share on X (Opens in new window) X
- Click to share on Pocket (Opens in new window) Pocket