Haijuzu kumfuata kichwa mchunga yeyote hii leo, pasi na kujali ni mtu gani. Tungelikuwa tunamfuata kichwa mchunga mtu, basi tungelimfata kibubusa imaam wa Ahl-us-Sunnah Ahmad bin Hanbal. Tungelimfuata kibubusa Abu Bakr as-Swiddiyq (Radhiya Allaahu ´anh). Hata hivo Allaah (´Azza wa Jall) anasema:
وَمَا آتَاكُمُ الرَّسُولُ فَخُذُوهُ وَمَا نَهَاكُمْ عَنْهُ فَانتَهُوا ۚ وَاتَّقُوا اللَّـهَ ۖ إِنَّ اللَّـهَ شَدِيدُ الْعِقَابِ
”Kile anachokupeni Mtume, basi kichukueni, na kile anachokukatazeni, basi kiacheni. Mcheni Allaah; hakika Allaah ni mkali wa kuadhibu.”[1]
فَلَا وَرَبِّكَ لَا يُؤْمِنُونَ حَتَّىٰ يُحَكِّمُوكَ فِيمَا شَجَرَ بَيْنَهُمْ ثُمَّ لَا يَجِدُوا فِي أَنفُسِهِمْ حَرَجًا مِّمَّا قَضَيْتَ وَيُسَلِّمُوا تَسْلِيمًا
“Naapa kwa Mola wako! Hawatoamini mpaka wakufanye wewe ni hakimu katika yale wanayozozana kati yao kisha wasipate katika nyoyo zao uzito katika yale uliyohukumu na wajisalimishe kwa kujisalimisha.”[2]
Sijioni kuwa ninastahiki kufuatwa, wala sioni kuwa maoni yangu yanatakiwa kuwa suala la mjadala. Naamini kuwa anayemfuata kichwa mchunga yeyote hii leo basi ameangamia. Nataka angalau kwa uchache uwe kama Haafidhw Ibn Kathiyr, Haafidhw Ibn Hajar, Shaykh-ul-Islaam Ibn Taymiyyah, Haafidhw Ibn-ul-Qayyim, Imaam al-Bukhaariy, Imaam Maalik na wanazuoni wetu wa zamani – Allaah awarehemu! Ama kumfata kibubusa mtu wa leo ambao amehifadhi Hadiyth kumi au ambaye ni mfaswaha haifai. Mfuate Mola wako na Sunnah za Mtume wako Muhammad (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam).
[1] 59:07
[2] 4:65
- Muhusika: ´Allaamah Muqbil bin Haadiy al-Waadi´iy
- Tarjama: Firqatunnajia.com
- Marejeo: Qam´-ul-Mu´aanid, uk. 410-411
- Imechapishwa: 08/07/2025

Muhusika: ´Allaamah Muqbil bin Haadiy al-Waadi´iy
Tarjama: Firqatunnajia.com
Marejeo: Qam´-ul-Mu´aanid, uk. 410-411
Imechapishwa: 08/07/2025
https://firqatunnajia.com/kama-tungelimfuata-yeyote-kichwa-mchunga/