Swali: Kuna watu wana kawaida wanapotaka kuswali Dhuhaa wanaita mtu mwingine au watu wawili?

Jibu: Sijui msingi wa hilo. Lakini ikitokea kwa bahati mbaya hapana neno. Lakini kule kuchunga kwake jambo hilo sijui msingi wake. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alimtembelea bibi yake Anas na akaswalisha ambapo mayatima na Anas wakaswali nyuma yake na bibi kizee yule akawa nyuma yao. Vilevile alimtembelea ´Utbaan baada ya kumwita amfanyie mahali pa kuswalia akaswali yale maeneo anayotaka ´Utbaan.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/23610/حكم-تحري-الجماعة-في-صلاة-الضحى
  • Imechapishwa: 29/02/2024