Dhikr kwa sauti ya juu baada ya kusoma Suurah “adh-Dhuhaa”s

Swali: Baada ya imamu kusoma Suurah “adh-Dhuhaa” katika Tarawiyh, aliwaamrisha waswaliji kusema kwa sauti:

لا إِلهَ إِلاَّ الله

“Hapana mungu wa haki isipokuwa Allaah.”

الله أَكبر

“Allaah ni mkubwa.”

الْحَمْدُ لله

“Himdi zote njema anastahiki Allaah.”

Anadai kuwa ni Sunnah na kwamba Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) aliwaamrisha Maswahabah zake kumshukuru Allaah wakati uliposimama wahy. Ni ipi hukumu ya hilo?

Jibu: Ni kweli ipo Hadiyth katika jambo hilo, lakini ni dhaifu. Haafidhw adh-Dhahabiy ameitaja katika “Twabaqaat-ul-Qurraa´ al-Kibaar” na akasema kuwa katika cheni yake ya wapokezi yuko Abiy Bazzah. Sio al-Qaasim bin Abiy Bazzah, isipokuwa mjukuu wake Ahmad bin Muhammad. Kwa hivyo Hadiyth haikuthibiti kutoka kwa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam). Kwa maana nyingine ni Bid´ah kusema hivo.

  • Muhusika: ´Allaamah Muqbil bin Haadiy al-Waadi´iy
  • Tarjama: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Qam´-ul-Mu´aanid, uk. 311-312
  • Imechapishwa: 11/05/2025