Imesuniwa kusema aina ya kila Takbiyr mbili:

الله أكبر كبيرا، والحمد لله كثيرا، وسبحان الله بكرة وأصيلا، وصلى الله على محمد النبي وآله وسلم تسليما كثيرا

”Allaah ni mkubwa kwelikweli, himdi za Allaah kwa wingi, himdi nyingi ni Zake Allaah, Allaah ametakasika asubuhi na jioni, swalah na amani zimwendee Mtume, kizazi chake na awasalimishe kwelikweli.”

Hilo ni kutokana na maneno ya ´Uqbah bin ´Aamir ambaye amesema:

”Nilimuuliza Ibn Mas´uud nini anachotakiwa kusema mtu baada ya Takbiyraat ambapo akajibu:

”Amhimidi Allaah, amsifu na amswalie Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam).”

al-Bayhaqiy pia amepokea kwa cheni ya wapokezi wake kutoka kwa Ibn Mas´uud kwa maneno na matendo.

Hudhayfah amesema:

”Abu ´Abdir-Rahmaan amesema kweli.”

Ni sawa pia endapo atasoma Adhkaar nyingine mbali na iliyotajwa juu. Kwani mahali hapo hakuna Adhkaar maalum.

Ibn-ul-Qayyim amesema:

”Alikuwa (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) akinyamaza baina ya kila Takbiyr mbili kinyamazo kidogo. Hakukuhifadhiwa kutoka kwake Dhikr maalum kati ya Takbiyraat.”

Akitilia shaka juu ya idadi ya Takbiyraat basi atajengea juu ya yakini ambayo ni ile idadi ya chini kabisa. Akisahau zile Takbiyr zenye kuzidi mpaka akaanza kusoma basi zimedondoka. Ni jambo lililopendekezwa imekwishapita mahali pake.

Mtu akijiunga na imamu baada ya kwamba amekwishaanza kusoma hatosoma zile Takbiyr zenye kuzidi. Vivyo hivyo akiunga naye kwenye Rukuu´. Katika hali hiyo ataleta Takbiyrat-ul-Ihraam kisha ndio aende katika Rukuu´. Asijishughulishe kulipe zile Takbiyr zilizompita.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Mulakhaswsw-ul-Fiqh (01/273)
  • Imechapishwa: 29/07/2020