3- Abu Hurayrah (Radhiya Allaahu ´anh) amesimulia kwamba Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:
“Jiepusheni na dhambi saba zenye kuangamiza.” Wakasema: “Ee Mtume wa Allaah! Ni yepi hayo?” Akasema: “Ni kumshirikisha Allaah, uchawi, kuiua nafsi ambayo Allaah kaiharamisha kuuliwa isipokuwa kwa haki, kula ribaa, kula mali ya mayatima, kukimbia siku ya vita na kuwazulia uongo wa kuzini wanawake waumini waghafilikaji na waliohifadhika.”
Kubwa katika hayo ni shirki. Kisha kunafuata uchawi kwa sababu mara nyingi unatokamana na shirki. Kwani uchawi una maana ya kuwaabudu majini na kuwaomba msaada na kujikurubisha kwao. Baada ya hapo kunafuatia kuiua nafsi ambayo imeharamishwa na Allaah isipokuwa kwa haki, riba, kukimbia siku ya vita ambapo yamekutana makundi mawili katika safu ana kwa ana ambapo mtu akalikimbia kundi lake na kuwatuhumu machafu wanawake waumini wenye kujihifadhi. Tuhuma hapa inahusiana na uchafu wa uzinzi.
Wameitwa waghafilikaji kwa sababu mara nyingi huwa hawatambui waliowatuhumu. Hukumu hiyohiyo inahusiana na wanaume wenye kujihifadhi. Hii ni dhambi kubwa. Mtuhumu anastahiki kusimamishiwa adhabu. Lakini hili mara nyingi linakuwa kwa wanawake. Ndio maana yule mwenye kuwatuhumu anatakiwa kuadhibiwa.
- Muhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
- Tarjama: Firqatunnajia.com
- Marejeo: Sharh Kitaab-it-Tawhiyd, uk. 88-89
- Imechapishwa: 09/12/2018
Mshirikishe mwenzako:
- Click to share on Telegram (Opens in new window)
- Click to share on WhatsApp (Opens in new window)
- Click to print (Opens in new window)
- Click to email a link to a friend (Opens in new window)
- Click to share on Facebook (Opens in new window)
- Click to share on Twitter (Opens in new window)
- Click to share on Pocket (Opens in new window)
Related
Hakuna mafanikio ya ribaa
Allaah (´Azza wa Jall) amesema: يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا لَا تَأْكُلُوا الرِّبَا أَضْعَافًا مُّضَاعَفَةً ۖ وَاتَّقُوا اللَّـهَ لَعَلَّكُمْ تُفْلِحُونَ ”Enyi walioamini! Msile ribaa mkizidisha maradufu juu ya maradufu; na mcheni Allaah mpate kufaulu.”[1] Aayah hii inakataza kula ribaa na kwamba ni moja katika sababu za kufaulu. Kuacha kula ribaa ni moja ya…
In "Ribaa"
24. Mlango kuhusu uchawi
Shaykh-ul-Islaam Muhammad bin ´Abdil-Wahhaab (Rahimahu Allaah) amesema: 1- Allaah (Ta´ala) amesema: وَلَقَدْ عَلِمُواْ لَمَنِ اشْتَرَاهُ مَا لَهُ فِي الآخِرَةِ مِنْ خَلاَقٍ “Kwa hakika wamekwishaelewa kwamba atakayenunua [kwa kujipatia elimu ya uchawi huo] hatopata katika Aakhirah fungu lolote.” (al-Baqarah 02:102) 2- أَلَمْ تَرَ إِلَى الَّذِينَ أُوتُوا نَصِيبًا مِّنَ الْكِتَابِ يُؤْمِنُونَ بِالْجِبْتِ…
In "Sharh Kitaab-it-Tawhiyd - Ibn Baaz"
38. Kubwa ambalo Allaah amewakataza waja ni shirki
Shaykh-ul-Islaam Muhammad bin ´Abdil-Wahhaab (Rahimahu Allaah) amesema: Kubwa Alilokataza Allaah ni Shirki, nako ni kuomba wengine pamoja Naye. MAELEZO Kubwa alilokataza Allaah... – Hii ni faida kubwa. Kwani wapo watu wanaoamini kwamba yapo mambo ambayo ndio maovu makubwa na ndio makubwa ambayo Allaah amekataza na utawasikia wakisema kuwa ribaa na…
In "Sharh Thalaathat-il-Usuwl – al-Fawzaan"