Swali: Baadhi ya watu wana madeni na hawajahiji ile hajj ya kwanza. Lakini hajj upande wake mtu huyo haimgharimu sana kwa sababu anachochukua ni hema na chakula kutoka nyumbani mwao. Hakuna kitachowagharimu isipokuwatu bei ya mafuta. Kama ataongozana na mashirika basi hakuna atachotoa isipokuwa tu takriban Riyaal ishirini. Je, katika hali hii hajj ni wajibu kwao?

Jibu: Sio wajibu kwao kufanya hajj. Midhali wako na madeni basi hajj sio wajibu kwao hata kama gharama zake zitakuwa ndogo. Isipokuwa pengine mtu ambaye anaenda pamoja na mahujaji ambapo atawatumikia na baadaye watampa malipo kwa sababu ya huduma hii, huyu tunaweza kusema kwamba amechuma mali ambayo anaweza kulipa deni lake kutoka hajj hii. Huyu tunaweza kumwambia kwamba ni sawa akahiji. Ama mtu ambaye hajj itamgharimu, japokuwa ni kitu kidogo, basi amshukuru Allaah juu ya afya na alipe deni lake kabla ya hajj.

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: al-Liqaa’ ash-Shahriy (53) http://binothaimeen.net/content/1204
  • Imechapishwa: 20/08/2019