Darsa kwa wasiojua kiarabu kabla ya Khutbah ya ijumaa

Swali: Katika msikiti wetu kwenye kituo cha Kiislamu huko (Marekani). Wasikilizaji ni ndugu zetu. Wana darsa kabla ya Khutbah ya siku ya ijumaa. Najua tangu hapo kitambo kwamba haifai kutoa darsa kabla ya Khutbah ya ijumaa.

al-Albaaniy: Ndio.

 Swali: Wanafanya hivo kwa sababu wasikilizaji hawazungumzi lugha ya kiarabu. Darsa inakuwa ni ile Khutbah imetarjumiwa kwa lugha ya kingereza. Je, jambo hilo linafaa?

al-Albaaniy: Unauliza juu ya hiyo Khutbah au darsa?

Muulizaji: Kuhusu hiyo darsa kabla ya Khutbah. Khutbah inatolewa kwa kiarabu.

al-Albaaniy: Darsa haijuzu. Hoja uliyotoa haitakasi kutoa darsa kabla ya Khutbah. Lakini hata hivyo wanaweza baada ya Khutbah na baada ya swalah au ndani ya Khutbah akawatangazia wasiokuwa waarabu wakamuuliza maswali au mambo yenye kutatiza baada ya swalah. Lakini kabla ya darsa ni jambo lisilofaa.

Muulizaji: Kama wanataka nitoe darsa kabla ya Khutbah ya ijumaa.

al-Albaaniy: Haijuzu.

  • Mhusika: Imaam Muhammad Naaswir-ud-Diyn al-Albaaniy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Silsilat-ul-Hudaa wan-Nuur (1023)
  • Imechapishwa: 10/12/2020