Swali: Kuna damu yenye kubaki kwenye nyama baada ya kuchinjwa. Ni najisi?

Jibu: Hapana. Haidhuru. Ni yenye kusamehewa. Damu yenye kubaki katika nyama inaliwa na haidhuru. Ni yenye kusamehewa. Damu ilio ya haramu ni ile yenye kuchuruzika kutoka kwenye mishipa ya koo wakati wa kuchinja. Damu kama hii ndio najisi.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh ´Umdat-il-Fiqh (02) http://www.alfawzan.af.org.sa/sites/default/files/omdh–14340204.mp3
  • Imechapishwa: 25/08/2020