Damu inayomtoka mfungaji wakati wa ajali

Swali: Mtu kutokwa na damu kinyume na matakwa yake kutokana na ajali au kukatika kunaharibu funga yake?

Jibu: Hakuharibu swawm yake damu ikimtoka pasi na kutaka kwake. Kwa mfano ameumia na akatokwa na damu au akatokwa na damu puani hakumfunguzi  kwa sababu sio kwa kutaka kwake. Hata kama itakuwa nyingi hakumfunguzi. Kinachofunguza ni kuumika na kutiririkwa na damu. Amekusudia kuitoa damu na hivyo kunamfunguza. Kumepokelewa Hadiyth zinazungumzia mwenye kufanya chuku na mwenye kufanyiwa.

Swali: Je, hili linalinganishwa (يقاس) mtu akajitolea damu mchana wa Ramadhaan?

Jibu: Ndio. Akijitolea damu nyingi basi kunamfunguza. Kwa sababu anakuwa mfano wa aliyefanya chuku.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Majmuu´-ul-Fataawaa (02/396)
  • Imechapishwa: 15/03/2022