Daktari wa kiume, mgonjwa wa kike

Swali: Je, inafaa kwa mwanamke kujifunua baadhi ya maeneo ya mwili wake mbele ya daktari wa kiume pamoja na kuwepo wauguzi wengine pamoja nao?

Jibu: Haijuzu kwa mwanaume kufunua mwili wa mwanamke isipokuwa ikiwa hakuna daktari bingwa. Hapo ndipo itafaa kwa ajili ya dharurah mwanaume akamfunua. Wakiwa pamoja na wauguzi wengine, basi inaondoke ile faragha.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh ´Umdat-il-Fiqh (42)
  • Imechapishwa: 03/07/2024