Swali: Ikiwa mtu yuko ndani ya swalah kisha akapiga chafya, je, amsifu Allaah, ni mamoja iwe ni swalah ya faradhi au ya Sunnah?

Jibu: Ndiyo, imesuniwa kwake kumhimidi Allaah. Hii ni kwa sababu imethibiti katika Hadiyth Swahiyh kwamba Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alimsikia mtu akimhimidi Allaah baada ya kupiga chafya akiwa katika swalah na hakumkataza. Bali alisema:

”Nimeona Malaika kadhaa wakiharakia ambapo kila mmoja wao akitaka kuwa ndiye atakayeiandika.”

Jengine ni kwa sababu kumsifu Allaah ni katika aina ya Dhikr ya swalah na wala hakupingani na swalah.

  • Muhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Tarjama: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Majmuu´-ul-Fataawaa (29/352)
  • Imechapishwa: 14/03/2026