Cha kufanya wakati unapogundua kiungo fulani hakikupata maji ya wudhuu´

Swali: Je, mtu achukue maji mapya kwa ajili ya sehemu ambayo haikupata maji au apasugue kwa maji yaliyobaki mkononi?

Jibu: Ikiwa hakujapita muda mrefu tangu wudhuu´ wake, basi inatosha kuosha sehemu hiyo iliyokosa maji. Isipokuwa ikiwa inahusiana na mkono, basi anapaswa kuosha viungo vinavyofuata ili kupatikane ule mpangilio. Ataosha sehemu hiyo iliyokosa maji na viungo vinavyofuata ili kupatikane ule mpangilio. Lakini sehemu hiyo iliyokosa maji ni mguu inatosha kuosha mguu pasi na kitu kingine.

Swali: Watu wengine wakiona sehemu imekosa maji ndani ya swalah hutema mate na wakayaparaza na wanatosheka kufanya hivo?

Jibu: Hapana… Hili ni kosa. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alimwamrisha yule bwana kurudi kutawadha.

  • Muhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Tarjama: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/24732/كيفية-غسل-اللمعة-عند-الوضوء
  • Imechapishwa: 04/12/2024