Bora ni kuja mapema msikitini au kuswali Sunnah nyumbani kwanza?

Swali: Vipi kukusanya baina ya swalah ya kupendeza iswaliwe nyumbani na kuja mapema msikitini?

Jibu:

“Swalah bora ya mtu ni nyumbani isipokuwa swalah ya faradhi.”

Swalah ya Dhuhaa, swalah ya usiku na swalah za Rawaatib bora ni kuziswali nyumbani. Hata hivyo hapana vibaya mtu akiziswali msikitini.

Swali: Raatibah inayoswaliwa kabla ya swalah bora ni kuiswali msikitini au nyumbani?

Jibu: Yote ni yenye kuenea, Hadiyth ni yenye kuenea. Anaweza kuiswali nyumbani kisha akaja msikitini kuswali swalah ya mamkizi ya msikiti. Akikusudia kuja mapema ana mashiko na katika hali hiyo ataiswali msikitini ili aweze kuwahi safu ya kwanza au kuwa karibu na imamu. Jambo ni lenye wasaa. Lengo lake ni jema kuwa karibu na imamu au awe katika safu ya kwanza. Baadhi ya misikiti inakuwa yenye kujaa kutokana na wingi wa waswaliji. Kwa hivyo akija mapema wakati au kabla ya adhaana ili awahi safu ya kwanza pengine kufanya hivo ndio bora kwa upande huo. Lengo ni kushindana kwa ajili ya safu ya kwanza. Kuhusu swalah ya sunnah inayoswaliwa baada ya swalah ya faradhi bora ni kuiswali nyumbani.

  • Muhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Tarjama: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/24173/هل-الافضل-التبكير-للمسجد-ام-التنفل-في-البيت
  • Imechapishwa: 12/09/2024