Bora kwa msafiri ni kufupisha lakini kuswali kila swalah kwa wakati wake

Swali: Baadhi ya watu wanaposafiri kwa mfano kutoka Riyaadh kwenda al-Kharj, umbali wa takriban 80 km, huswali wakiwa njiani kwa kukusanya swalah. Je, kitendo chao ni sahihi?

Jibu: Msafiri anaruhusiwa kukusanya swalah na pia anaruhusiwa kuswali kila swalah katika wakati wake. Lakini ikiwa ni mkazi, basi bora zaidi ni kuswali kila swalah ndani ya wakati wake. Hivo ndivo alivyofanya Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) huko Minaa katika hijjah ya kuaga.

  • Muhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Tarjama: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Majmuu´-ul-Fataawaa (30/209)
  • Imechapishwa: 15/03/2026