Swali: Ikiwa niko safarini na ninataka kukusanya swalah, je, lililo bora ni kukusanya mwanzo wa wakati au mwisho wa wakati?
Jibu: Lililo bora ni kufanya lililo rahisi zaidi kwako na kwa marafiki zako. Ikiwa umekaa mahali kwa kukaa kusikokuzuia kufupisha na kukusanya swalah, basi kuacha kukusanya ni bora zaidi. Kwa maana nyingine wewe na marafiki zako mswali kila swalah ndani ya wakati wake. Hivi ndivyo alivyofanya Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) katika hijjah ya kuaga alipokuwa Minaa. Ama ikiwa uko safarini unaendelea na safari, basi lililo bora ni kukusanya mwanzo wa wakati, ikiwa utaondoka baada ya kuingia wakati wa swalah ya kwanza. Ikiwa kuondoka kwako ni kabla ya kuingia wakati wa swalah ya kwanza, basi lililo bora ni kukusanya mwisho wa wakati. Hii ni kwa sababu imethibiti kutoka kwa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) katika Hadiyth ya Anas (Radhiya Allaahu ´anh) na wengineo yanayofahamisha juu ya hilo.
- Muhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
- Tarjama: Firqatunnajia.com
- Marejeo: Majmuu´-ul-Fataawaa (30/214)
- Imechapishwa: 15/03/2026
Swali: Ikiwa niko safarini na ninataka kukusanya swalah, je, lililo bora ni kukusanya mwanzo wa wakati au mwisho wa wakati?
Jibu: Lililo bora ni kufanya lililo rahisi zaidi kwako na kwa marafiki zako. Ikiwa umekaa mahali kwa kukaa kusikokuzuia kufupisha na kukusanya swalah, basi kuacha kukusanya ni bora zaidi. Kwa maana nyingine wewe na marafiki zako mswali kila swalah ndani ya wakati wake. Hivi ndivyo alivyofanya Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) katika hijjah ya kuaga alipokuwa Minaa. Ama ikiwa uko safarini unaendelea na safari, basi lililo bora ni kukusanya mwanzo wa wakati, ikiwa utaondoka baada ya kuingia wakati wa swalah ya kwanza. Ikiwa kuondoka kwako ni kabla ya kuingia wakati wa swalah ya kwanza, basi lililo bora ni kukusanya mwisho wa wakati. Hii ni kwa sababu imethibiti kutoka kwa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) katika Hadiyth ya Anas (Radhiya Allaahu ´anh) na wengineo yanayofahamisha juu ya hilo.
Muhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
Tarjama: Firqatunnajia.com
Marejeo: Majmuu´-ul-Fataawaa (30/214)
Imechapishwa: 15/03/2026
https://firqatunnajia.com/bora-kwa-msafiri-kukusanya-mwanzo-au-mwisho-wa-wakati/