Bora kutumia ”Sijui” badala ya ”Haijapokelewa kwa Mtume”

Swali: Wakati muftiy au imamu anaposema:

”Sijui kama jambo hilo limepokelewa kutoka kwa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam).”

Je, anamaanisha kwa upeo wa elimu yake?

Jibu: Ikiwa atasema kwamba hajui, hilo ni jambo zuri. Lakini tatizo linakuja pale ataposema kwamba haijapokelewa kutoka kwa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam). Haitakikani kutumia msemo ”Haijapokelewa” hata kama anamaanisha kwa upeo wa elimu yake. Badala yake anaweza kutumia neno ”Sijui, ”Sifahamu hilo” au ”Sijakutana na chochote katika suala hili” au maneno yanayofanana na hayo.

  • Muhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Tarjama: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/25062/ما-حكم-قول-المفتي-او-الامام-ما-ورد-كذا-عن-الرسول
  • Imechapishwa: 27/01/2025