Allaah alimtaka Abu Lahab aamini kilimwengu au kishari´ah?

Swali: Allaah (Subhaanahu wa Ta´ala) alimtaka Abu Lahab kuamini kilimwengu au kishari´ah?

Jibu: Kishari´ah. Lau angekuwa ametaka aamini kimaumbile, basi angeliamini. lakini Allaah hakumtaka  kimaumbile. Allaah ametaka watu wote waamini kishari´ah. Lakini yule anayemtaka kimaumbile ni lazima itokee. Kwa hivyo Abu Taalib na Abu Lahab walitakiwa kuwa waislamu kishari´ah, lakini hawakukubali. Ama matakwa ya kimaumbile, tayari lilikuwa limepita katika ujuzi wa Allaah kwamba hawatasilimu.

  • Muhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Tarjama: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/25047/هل-اراد-الله-الايمان-من-ابي-لهب-كونا-او-شرعا
  • Imechapishwa: 27/01/2025