Bora kumsifu Allaah au kuomba du´aa za jumla?

Swali: Je, kumsifu Allaah ni bora zaidi kuliko du´aa?

Jibu: Kumsifu ndio bora zaidi, kwani sifa ni aina ya Dhikr. Lakini pale kunapokuwa na haja ya kufanya du´aa, basi du´aa huwa bora zaidi. Mfano wa hayo ni kama du´aa ya Istikhaarah, du´aa ya kusema:

رب اغفر لي

”Mola, nisamehe.”

baina ya sijda mbili na kuomba du´aa katika sujuud. Maeneo hayo ni bora kuliko kisomo.

  • Muhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Tarjama: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/31208/هل-الثناء-على-الله-اعظم-من-الدعاء
  • Imechapishwa: 11/10/2025