Swali: Baada ya mvua kuongezeka siku hizi, ni ipi hukumu ya kukusanya swalah ya Maghrib pamoja na ´Ishaa wakati mvua inanyesha katika wakati wa Maghrib? Ni lipi lililo bora; kukusanya au kutokusanya?
Jibu: Hili hutofautiana. Ikiwa mvua ni nyingi kwa kiasi kinachowaudhi wapita njia, basi hilo linafanya kukusanya kuwa halali, kukusanya swalah ya Maghrib na ´Ishaa, na kwa mujibu wa maoni sahihi pia Dhuhr na ´Aswr pale panapohitajika. Ama ikiwa ni kitu chepesi na hakuna kuteleza katika masoko yaliyopigwa lami na kutengenezwa na mvua ni kidogo isiyoudhi, basi hakuna kukusanya. Unaswali kila swalah ndani ya wakati wake. Lakini ikiwa ugumu umetokana na mvua au kuteleza katika masoko, basi hakuna tatizo kukusanya.
- Muhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
- Tarjama: Firqatunnajia.com
- Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/2155/حكم-جمع-الصلاة-وقت-هطول-الامطار
- Imechapishwa: 13/03/2026
Swali: Baada ya mvua kuongezeka siku hizi, ni ipi hukumu ya kukusanya swalah ya Maghrib pamoja na ´Ishaa wakati mvua inanyesha katika wakati wa Maghrib? Ni lipi lililo bora; kukusanya au kutokusanya?
Jibu: Hili hutofautiana. Ikiwa mvua ni nyingi kwa kiasi kinachowaudhi wapita njia, basi hilo linafanya kukusanya kuwa halali, kukusanya swalah ya Maghrib na ´Ishaa, na kwa mujibu wa maoni sahihi pia Dhuhr na ´Aswr pale panapohitajika. Ama ikiwa ni kitu chepesi na hakuna kuteleza katika masoko yaliyopigwa lami na kutengenezwa na mvua ni kidogo isiyoudhi, basi hakuna kukusanya. Unaswali kila swalah ndani ya wakati wake. Lakini ikiwa ugumu umetokana na mvua au kuteleza katika masoko, basi hakuna tatizo kukusanya.
Muhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
Tarjama: Firqatunnajia.com
Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/2155/حكم-جمع-الصلاة-وقت-هطول-الامطار
Imechapishwa: 13/03/2026
https://firqatunnajia.com/bora-kukusanya-swalah-wakati-wa-mvua-au-kutokukusanya/