Bora kujitahidi kumwabudu Allaah badala ya kuoa?

Swali: Allaah (Ta´ala) amesema:

وَتَبَتَّلْ إِلَيْهِ تَبْتِيلًا

”… na jipinde Kwake kwa kujitolea ipasavyo.” (73.08)

Jibu: Kwa maana ya kufanya ´ibaadah. Kwa msemo mwingine ajitahidi kumwabudu Yeye (Jalla wa ´Alaa). Haina maana kwamba aache matendo.

Swali: Anayesema kuwa mtu akijitahidi kumwabudu Allaah na kuwatendea wema wazazi ni bora kuliko kuoa?

Jibu: Ajibiwe na kubainishiwa kuwa huo ni ujinga. Allaah ameamrisha kuoa pale aliposema:

وَأَنكِحُوا الْأَيَامَىٰ مِنكُمْ

“Waozesheni wajane miongoni mwenu… “ (24:32)

فَانكِحُوا مَا طَابَ لَكُم مِّنَ النِّسَاءِ

“Basi oeni waliokupendezeni katika wanawake wengine.” (04:03)

Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) pia ameamrisha hilo. Hakuna maneno ya yeyote yanayokuwa juu ya maneno ya Allaah na Mtume Wake. Maneno yanayokwenda kinyume na maneno ya Allaah na Mtume wake ni lazima kuyatupilia mbali.

Swali: Vipi Maryam kuitwa Butuul?

Jibu: Kwa maana kwa ajili ya kufanya ´ibaadah.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/23824/حكم-ترك-العمل-والزواج-للانشغال-بالعبادة
  • Imechapishwa: 15/05/2024