Swali: Bora ni kuchinja katika ´Iyd-ul-Adhwhaa au kutoa swadaqah thamani yake?

Jibu: Kuchinja ndio bora. Ikiwa mtu atauliza kama bora ni kutoa swadaqah 500 SAR au achinje? Bora ni kuchinja. Ikiwa atasema kuwa kwa pesa hizo anaweza kununua nyama nyingi kuliko thamani ya kondoo na mbuzi mara nne au mara  tano, je, bora afanye hivo au chinje? Bora ni kuchinja. Kuchinja ndio bora kuliko kutoa swadaqah ile thamani yake. Aidha ndio bora kuliko kununua nyama kwa kiwango chake au zaidi yake ili aitoe swadaqah. Hivo ni kwa sababu lengo muhimu zaidi katika kuchinja ni kule kumwabudu Allaah (Ta´ala). Amesema (Ta´ala):

لَن يَنَالَ اللَّـهَ لُحُومُهَا وَلَا دِمَاؤُهَا وَلَـٰكِن يَنَالُهُ التَّقْوَىٰ مِنكُمْ

”Haimfikii Allaah nyama zake wala damu yake, lakini unamfikia uchaji kutoka kwenu.”[1]

[1] 22:37

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh-ul-Mumti´ (07/481)
  • Imechapishwa: 18/07/2020