Swali: Bora ni kuchinja katika ´Iyd-ul-Adhwhaa au kutoa swadaqah thamani yake?
Jibu: Kuchinja ndio bora. Ikiwa mtu atauliza kama bora ni kutoa swadaqah 500 SAR au achinje? Bora ni kuchinja. Ikiwa atasema kuwa kwa pesa hizo anaweza kununua nyama nyingi kuliko thamani ya kondoo na mbuzi mara nne au mara tano, je, bora afanye hivo au chinje? Bora ni kuchinja. Kuchinja ndio bora kuliko kutoa swadaqah ile thamani yake. Aidha ndio bora kuliko kununua nyama kwa kiwango chake au zaidi yake ili aitoe swadaqah. Hivo ni kwa sababu lengo muhimu zaidi katika kuchinja ni kule kumwabudu Allaah (Ta´ala). Amesema (Ta´ala):
لَن يَنَالَ اللَّـهَ لُحُومُهَا وَلَا دِمَاؤُهَا وَلَـٰكِن يَنَالُهُ التَّقْوَىٰ مِنكُمْ
”Haimfikii Allaah nyama zake wala damu yake, lakini unamfikia uchaji kutoka kwenu.”[1]
[1] 22:37
- Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
- Mfasiri: Firqatunnajia.com
- Marejeo: Sharh-ul-Mumti´ (07/481)
- Imechapishwa: 18/07/2020
Swali: Bora ni kuchinja katika ´Iyd-ul-Adhwhaa au kutoa swadaqah thamani yake?
Jibu: Kuchinja ndio bora. Ikiwa mtu atauliza kama bora ni kutoa swadaqah 500 SAR au achinje? Bora ni kuchinja. Ikiwa atasema kuwa kwa pesa hizo anaweza kununua nyama nyingi kuliko thamani ya kondoo na mbuzi mara nne au mara tano, je, bora afanye hivo au chinje? Bora ni kuchinja. Kuchinja ndio bora kuliko kutoa swadaqah ile thamani yake. Aidha ndio bora kuliko kununua nyama kwa kiwango chake au zaidi yake ili aitoe swadaqah. Hivo ni kwa sababu lengo muhimu zaidi katika kuchinja ni kule kumwabudu Allaah (Ta´ala). Amesema (Ta´ala):
لَن يَنَالَ اللَّـهَ لُحُومُهَا وَلَا دِمَاؤُهَا وَلَـٰكِن يَنَالُهُ التَّقْوَىٰ مِنكُمْ
”Haimfikii Allaah nyama zake wala damu yake, lakini unamfikia uchaji kutoka kwenu.”[1]
[1] 22:37
Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
Mfasiri: Firqatunnajia.com
Marejeo: Sharh-ul-Mumti´ (07/481)
Imechapishwa: 18/07/2020
https://firqatunnajia.com/bora-kuchinja-au-kutoa-swadaqah/
Mshirikishe mwenzako:
- Click to share on Telegram (Opens in new window)
- Click to share on WhatsApp (Opens in new window)
- Click to print (Opens in new window)
- Click to email a link to a friend (Opens in new window)
- Click to share on Facebook (Opens in new window)
- Click to share on Twitter (Opens in new window)
- Click to share on Pocket (Opens in new window)