Bid´ah ni khabithi na zinauharibu Uislamu na Waislamu. Kwa ajili ndio ndio maana unakuta vitabu vimebainisha hali ya Khawaarij, Murji-ah, Mu´tazilah, Rawaafidhw na wengineo kutokana na khatari yao juu ya Uislamu.

Ni wajibu kwetu kuacha mielekeo hii ya kisiasa ambayo inauchuja Uislamu na inataka kuwakusanya na kuwafanya Waislamu kuwa na umoja pasi na kujali ni hali gani watayokuwemo. Ukusanyaji huu sio wa sawa.

Tunawakusanya watu katika Qur-aan na Sunnah. Ama kuwakusanya juu ya Huluul, Wahdat-ul-Wujuud, ar-Rafdhw, kuabudu makaburi na juu ya ´Aqiydah za kikafiri ambazo zina ukafiri zaidi kuliko za kiyahudi na za kinaswara. Tuwafanye watu wawe na umoja juu ya hili na kusema huu ndio Uislamu?! Huu ndio upotevu.

Kwa ajili hii, Waislamu wanatakiwa kuielewa Dini yao na kujaribu kuwatakasa waislamu na kuwasafisha na kuwalea watu juu ya Dini ya Allaah ya haki ili waweze kupata karama na ushindi kutoka kwa Allaah (Tabaarak wa Ta´ala) na vilevile nusura duniani na uokovu na furaha Aakhirah.

  • Mhusika: ´Allaamah Rabiy´ bin Haadiy al-Madkhaliy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: adh-Dhariy´ah ilaa Bayaan Maqaasid Kitaab-ish-Sharï´ah (1/151)
  • Imechapishwa: 19/05/2015