Bid´ah ya kusalimiana baada ya swalah

Swali: Ni ipi hukumu ya kusalimia upande wa kulia na upande wa kushoto baada ya swalah?

Jibu: Kuhusu yale yanayofanywa na baadhi ya watu ambapo baada tu ya kumaliza kutoa salamu kuliani na kushotoni wanapeana mikono na wale walioko upande wa kulia na walioko upande wa kushoto maimamu wamesema kuwa jambo hilo ni Bid´ah. Lakini ikiwa mtu atasubiri baada ya kumaliza kusoma Adhkaar kukiwemo Tahliyl na Tasbiyh kisha akataka kuwasilimia walioko upande wa kulia na upande wa kushoto hakuna neno. Ikiwa walikuwa hawajaonana ni sawa akafanya hivo. Lakini pale tu anapomaliza kutoa salamu upande wa kuliani mwake na upande wa kushotoni mwake anapeana mikono na wale walioko nyuma yake na walioko kuliani mwake kitendo hichi ni Bid´ah na hakina msingi wowote. Kilichowekwa katika Shari´ah ni mtu kusema:

أستغفر الله

”Namuomba Allaah msamaha.”

mara tatu. Aseme:

اللهم أنت السلام ومنك السلام

“Ee Allaah! Hakika wewe ndiye as-Salaam. Amani inatoka Kwako.”

Kisha aseme “Laa ilaaha illa Alllaah”, “Subhaan Allaah” na “Allaahu Akbar”. Baada ya haya akitaka kusalimia ni sawa.

  • Mhusika: ´Allaamah ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah ar-Raajihiy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Fataawaa Mutanawwi´ah (05) http://audio.islamweb.net/audio/index.php?page=FullContent&audioid=191110#219240
  • Imechapishwa: 28/10/2018