Swali: Je, Bid´ah si inaingia ndani ya utashi wa Allaah muda wa kuwa si ya ukafiri?
Jibu: Bid´ah haingii ndani ya matakwa ya Allaah. Mwenye nayo ni mwenye kutishiwa Moto isipokuwa ikiwa kama atatubia. Lakini Bid´ah hiyo ikiwa ni chini ya shirki bado kuna matarajio kwa yule mwenye nayo. Kwa sababu Bid´ah hiyo kwa upande fulani itakuwa ni yenye kuingia katika maana ya maasi lakini hata hivyo si yenye kuingia katika maneno Yake (Ta´ala):
إِنَّ اللَّـهَ لَا يَغْفِرُ أَن يُشْرَكَ بِهِ وَيَغْفِرُ مَا دُونَ ذَٰلِكَ لِمَن يَشَاءُ ۚ
“Hakika Allaah hasamehi kushirikishwa lakini anasamehe yaliyo chini ya hayo kwa amtakae.”
Ikiwa uzushi wa mzushi ni chini ya shirki basi una hukumu moja sawa na maasi kwa upande wa kwamba Allaah hatomdumisha mwenye nayo Motoni.
- Muhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
- Tarjama: Firqatunnajia.com
- Marejeo: Sharh Fadhwl-il-Islaam, uk. 25-26
- Imechapishwa: 29/05/2021
Mshirikishe mwenzako:
- Click to share on Telegram (Opens in new window)
- Click to share on WhatsApp (Opens in new window)
- Click to print (Opens in new window)
- Click to email a link to a friend (Opens in new window)
- Click to share on Facebook (Opens in new window)
- Click to share on Twitter (Opens in new window)
- Click to share on Pocket (Opens in new window)