Bid´ah ya matanga inatakiwa kutokomezwa

Swali: Ni vipi tutatokomeza Bid´ah hii ambayo inatokea kwenye vilio ambapo kunatengwa chakula na kukaa kwa mfiwa kwa muda wa siku tatu? Sisi tuko kwenye kijiji ambacho wanafanya kitendo hichi. Je, tufunge milango siku za kutoa pole?

Jibu: Kwa masikitiko makubwa haya hayafanywi kwenye kijiji chenu tu. Haya yanapatikana hata Riyaadh pia. Yameenea katika miji ya Saudi Arabia. Ni jambo lisilokuwa na asli. Lililo la wajibu ni watu kuachana nayo.

Sunnah ni kuwafanyia wafiwa chakula kwa kiasi cha kuwatosha tu. Ni wenye kushughulishwa na msiba, kama alivyoamrisha Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam). Ama kuzidisha juu ya hayo, kutengeneza chakula, watu kukaa siku kadhaa, yote haya ni katika shari na ni mambo yasiyofaa waliyowalazimisha nayo watu. Ni wajibu kuachana na mambo haya.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: at-Tafsiyr al-Mufasswal (54) http://www.alfawzan.af.org.sa/sites/default/files/tf–1431-11-03.mp3
  • Imechapishwa: 21/08/2020