Swali: Bibi yangu ni mwanamke mwenye kufanya ´ibaadah nyingi, lakini swalah yake si sahihi. Nimejaribu kumweleza lakini anasema kwamba amejifunza kwa fulani na fulani. Ni ipi hukumu ya swalah yake?

Jibu: Jaribu kumsahihisha katika makosa aliyoyafanya kadiri ya uwezo wako. Ikiwa una ujuzi na una maarifa ya hukumu ya Allaah katika mambo uliyoyataja. Hivyo jaribu kumpa nasaha na umbainishie makosa aliyoyafanya. Ikiwa kwa mfano hasomi al-Faatihah, basi mfundishe. Ikiwa hasomi Tashahhud (Tahiyyaat), basi mfundishe. Ikiwa anafanya haraka katika Rukuu´ na sujuud, basi mfundishe. Mwambie kwamba kitendo chake hicho hakisihi. Aidha msomee Hadiyth za Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) ili atulie moyo wake, aelewe na afahamu.

  • Muhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Tarjama: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Majmuu´-ul-Fataawaa (29/343)
  • Imechapishwa: 13/03/2026