Swali: Je, zakaah ya mapambo ya dhahabu inatolewa kutokana na ile bei ya ununuzi au ni kutokana na thamani yake pale ambapo umefikia wakati wa kuitoa?

Jibu: Zakaah ya vito inakuwa kila mwaka. Wala haiwi kwa bei ya ununuzi. Mambo yalivyo ni kwamba inakuwa kwa thamani yake pale ambapo umefikia wakati wake wa kuitoa. Tukikadiria kuwa mwanamke amenunua dhahabu kwa pesa 10.000 na ulipofikia wakati wa kuitolea zakaah thamani yake ikashuka kwenda 5000, basi ataitolea zakaah ya 5000. Na kinyume chake; akinunua dhahabu kwa 5000 ambapo ulipofikia wakati wa kuitolea zakaah thamani yake ikapanda kwenda katika 10.000, basi ataitolea zakaah ya 10.000. Kwa sababu kipindi hicho ndio wakati wa uwajibu wa kutoa zakaah.

  • Muhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Tarjama: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Majmuu´-ul-Fataawaa (18/132)
  • Imechapishwa: 22/05/2026