Swali: Je, ni wajibu pesa iliyowekwa rehani kuitolea zakaah? Je, mkopo unatolewa zakaah?

Jibu: Ni wajibu pesa iliyowekwa rehani kuitolea zakaah ikiwa ni pesa ya zakaah. Lakini mweka rehani na mtoza deni wanatakiwa kukubaliana. Kwa mfano mtu anaweka rehani ya kondoo kwa mtu (kondoo wanatolewa zakaah), basi analazimika kondoo hao kuwatolea zakaah. Rehani haidondoshi uwajibu wa kutoa zakaah. Anatakiwa kuwatolea zakaah, lakini baada ya idhini ya mweka rehani.

Kuhusu mkopo, tumeshatangulia kusema kuwa ikiwa yule mkopeshaji ni tajiri basi analazimika mkopo wake kuutolea zakaah kila mwaka. Mkopeshaji masikini hatolei zakaah mkopo wake hata kama itachukua miaka kumi kabla ya kurudishiwa pesa yake. Atalipa zakaah ya mkopo wake baada ya kulipwa. Katika hali hiyo atatoa zakaah ya mwaka mmoja tu.

  • Muhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Tarjama: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Majmuu´-ul-Fataawaa (18/34)
  • Imechapishwa: 22/05/2026