Bakora wakati wa Khutbah kwa mujibu wa Ibn ´Uthaymiyn

Swali: Ni ipi hukumu Khatwiyb kuegemea juu ya bakora wakati wa Khutbah?

Jibu: Akiihitajia kwa sababu ya udhaifu ni Sunnah kwa sababu Sunnah ni kutoa Khtubah kwa kusimama. Kitu kinachomsaidia mtu juu ya Sunnah nacho ni Sunnah. Ama kukiwa hakuna haja ya kuegemea juu ya bakora basi hapana haja ya mtu kufanya hivo[1].

[1] Tazama https://firqatunnajia.com/bakora-wakati-wa-khutbah-kwa-mujibu-wa-al-albaaniy/

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Majmuu´-ul-Fataawaa (16/95)
  • Imechapishwa: 27/01/2019