Bakora wakati wa Khutbah kwa mujibu wa al-Albaaniy

Swali: Je, ni Sunnah kwa Khatwiyb kuegemea juu ya bakora?

Jibu: Hapana, sio Sunnah. Ikiwa anahitajia bakora kila wakati anapotembea na anapopanda juu na kukhutubu, hakuna neno. Hata hivyo sio Sunnah ikiwa atafanya hivo kwa kukusudia.

  • Mhusika: Imaam Muhammad Naaswir-ud-Diyn al-Albaaniy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Silsilat-ul-Hudaa wan-Nuur (325)