Swali: Ni ipi hukumu kuwafarikisha khaswa vijana wa Ahl-us-Sunnah na wengineo katika Ahl-us-Sunnah kwa ujumla ambapo baadhi yao wakawaita wengine baadhi ya majina bandia na mfarakano wa kimakundi?

Jibu: Hawawi ni katika Ahl-us-Sunnah isipokuwa wakiwa pamoja na hawagawanyiki. Midhali wote ni Ahl-us-Sunnah basi ni kundi moja. Wakiingia katika makundi hawawi tena Ahl-us-Sunnah. Ahl-us-Sunnah wal-Jamaa´ah hata kama kati yao kunaweza kutokea tofauti katika baadhi ya masuala ya Fiqh yanayotokana na Ijtihaad katika mataga. Muda wa kuwa ´Aqiydah yao ni moja bado ni kundi moja.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Ma´aalim Manhaj Ahl-is-Sunnah wal-Jamaa´ah, uk. 46
  • Imechapishwa: 29/05/2021