Swali: Baba yangu alikuwa mgonjwa ambapo akaniomba nimfanyie tiba ya kuchomwa moto. Baada ya muda akafariki kwa ugonjwa huo. Je, ninapata dhambi kwa hilo ikiwa sikumfanyia tiba hiyo?
Jibu: Ikiwa mtoto alimpeleka baba yake kwa madaktari au baba yake alimwomba amfanyie tiba ya kuchomwa na akahakikisha kuwa tiba hiyo inafaa, basi hakuna ubaya katika hilo na wala hana kitu juu yake ikiwa atafariki. Kwa sababu kuchomwa moto ni miongoni mwa sababu za kupona. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:
“Uponyaji uko katika mambo matatu: kuchoma kwa moto, kukatwa na chombo cha kutoa damu au kunywa asali.”
Makusudio ni kwamba ikiwa atafariki baada ya hapo haisemwi kuwa ni kwa sababu ya kuchomwa moto. Huyu muda wake umetimia. Wala hakuna ubaya juu yako katika kumtibu, kumfanyia tiba hiyo alipokuomba hilo, kumletea daktari au mfano wa hayo. Tunamuomba Allaah awafanikishe wote.
- Muhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
- Tarjama: Firqatunnajia.com
- Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/3376/حكم-العلاج-بالكي-وما-يترتب-عليه
- Imechapishwa: 20/08/2026
Swali: Baba yangu alikuwa mgonjwa ambapo akaniomba nimfanyie tiba ya kuchomwa moto. Baada ya muda akafariki kwa ugonjwa huo. Je, ninapata dhambi kwa hilo ikiwa sikumfanyia tiba hiyo?
Jibu: Ikiwa mtoto alimpeleka baba yake kwa madaktari au baba yake alimwomba amfanyie tiba ya kuchomwa na akahakikisha kuwa tiba hiyo inafaa, basi hakuna ubaya katika hilo na wala hana kitu juu yake ikiwa atafariki. Kwa sababu kuchomwa moto ni miongoni mwa sababu za kupona. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:
“Uponyaji uko katika mambo matatu: kuchoma kwa moto, kukatwa na chombo cha kutoa damu au kunywa asali.”
Makusudio ni kwamba ikiwa atafariki baada ya hapo haisemwi kuwa ni kwa sababu ya kuchomwa moto. Huyu muda wake umetimia. Wala hakuna ubaya juu yako katika kumtibu, kumfanyia tiba hiyo alipokuomba hilo, kumletea daktari au mfano wa hayo. Tunamuomba Allaah awafanikishe wote.
Muhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
Tarjama: Firqatunnajia.com
Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/3376/حكم-العلاج-بالكي-وما-يترتب-عليه
Imechapishwa: 20/08/2026
https://firqatunnajia.com/baba-yake-amefariki-baada-ya-kumfanyia-tiba-ya-kuchomwa-moto/