Baba hayuko radhi nami kuhama kutoka nyumbani

Swali: Ninataka kujitenga na familia yangu ili niishi mimi na watoto wangu katika nyumba yetu binafsi, lakini baba yangu haridhii hilo. Je, nikitoka hali wao hawaridhii itakuwa ni kuwaasi wazazi?

Jibu: Inafaa kwako uzingatie radhi zao na ujitahidi kuwaridhisha ili utoke kwa ridhaa yao. Ikiwa kukaa kwako nao kuna kumuasi Allaah, kwa sababu unadhuriwa na ndugu zako au wengine, basi hapana vibaya ukitoka. Lakini kutoka kwa ridhaa na msamaha wa wazazi, pamoja na kujitahidi kuwafurahisha, hilo ni bora zaidi kwako. Ikiwa hakuna sababu ya kukufanya utoke na wazazi wako wanakuhitaji, basi usitoke.

  • Muhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Tarjama: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/3290/حكم-مفارقة-الوالدين-في-سكن-مستقل-بدون-رضاهم
  • Imechapishwa: 07/08/2026