Swali: Mimi na baba yangu tulienda Hajj takriban miaka mitatu iliyopita. Baada ya kusimama ´Arafah tulielekea Muzdalifah na tukakaa hapo mpaka karibu nusu ya usiku, kisha tukakwenda Minaa. Kwa sababu tulikuwa na kundi lililosisitiza kuondoka wakati huo. Je, tuna kosa lolote kwa kufanya hivyo mapema?
Jibu: Hakuna ubaya – Allaah akitaka – ikiwa watu wataondoka baada ya nusu ya usiku kutoka Muzdalifah. Lakini lililo bora ni kubaki hapo mpaka aswali Fajr na amtaje Allaah baada ya Fajr, amhimidi, amsifu na amuombe mpaka kupambazuke, kisha aondoke kama alivyofanya Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) kabla ya kuchomoza jua. Hata hivyo Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) aliwapa ruhusa watu dhaifu kuondoka usiku kutoka Muzdalifah, kama wanawake, watoto na walioko pamoja nao miongoni mwa dhaifu kama wazee, wagonjwa na mfano wao. Hivyo aliye pamoja na dhaifu hukumu yake ni kama yao; anaondoka pamoja nao, anapiga mawe pamoja nao na hakuna ubaya katika hilo.
- Muhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
- Tarjama: Firqatunnajia.com
- Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/3286/التوجه-من-مزدلفة-الى-منى-بعد-منتصف-الليل
- Imechapishwa: 07/08/2026
Swali: Mimi na baba yangu tulienda Hajj takriban miaka mitatu iliyopita. Baada ya kusimama ´Arafah tulielekea Muzdalifah na tukakaa hapo mpaka karibu nusu ya usiku, kisha tukakwenda Minaa. Kwa sababu tulikuwa na kundi lililosisitiza kuondoka wakati huo. Je, tuna kosa lolote kwa kufanya hivyo mapema?
Jibu: Hakuna ubaya – Allaah akitaka – ikiwa watu wataondoka baada ya nusu ya usiku kutoka Muzdalifah. Lakini lililo bora ni kubaki hapo mpaka aswali Fajr na amtaje Allaah baada ya Fajr, amhimidi, amsifu na amuombe mpaka kupambazuke, kisha aondoke kama alivyofanya Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) kabla ya kuchomoza jua. Hata hivyo Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) aliwapa ruhusa watu dhaifu kuondoka usiku kutoka Muzdalifah, kama wanawake, watoto na walioko pamoja nao miongoni mwa dhaifu kama wazee, wagonjwa na mfano wao. Hivyo aliye pamoja na dhaifu hukumu yake ni kama yao; anaondoka pamoja nao, anapiga mawe pamoja nao na hakuna ubaya katika hilo.
Muhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
Tarjama: Firqatunnajia.com
Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/3286/التوجه-من-مزدلفة-الى-منى-بعد-منتصف-الليل
Imechapishwa: 07/08/2026
https://firqatunnajia.com/ametoka-muzdalifah-kwenda-minaa-kabla-ya-nusu-ya-usiku/