Baba hataki kumuozesha msichana mtalikiwa

Swali: Kuna mwanamke mtalikiwa Ufaransa ambaye anataka kuolewa. Baba yake anakataa pamoja na kujua kuwa yuko na wajomba wanaomuogopa baba yake. Unamnasihi nini mwanamke huyu?

Jibu: Huyu hana njia nyingine zaidi ya kwenda mahakamani. Mahakama ndio yatamuozesha ikiwa kama walii wake amekataa kumuozesha kwa mtu anayemridhia. Mahakama ndio yatamuozesha. Ikiwa anaishi katika nchi ambapo hakuna mahakama aende katika kituo (markaz) ya Kiislamu. Kituo cha Kiislamu ndio kinachukua sehemu ya mahakama. Wamuozeshe.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: http://www.alfawzan.af.org.sa/sites/default/files/liqo%20%20-%2021%20-%2008%20-%201435.mp3
  • Imechapishwa: 09/04/2015