Baadhi ya Rak´ah anasoma Basmalah kwa sauti ya juu na zengine anasoma kimyakimya

Swali: Kuna imamu mmoja katika kisimamo cha Ramadhaan alikuwa anasoma kama kawaida hasomi Basmalah kwa sauti ya juu katika Faatihah na Suurah nyenginezo. Lakini alipofika katika Suurah “al-Falaq” alisoma Basmalah kwa sauti ya juu. Vivyo hivyo katika Suurah “an-Naas”. Je, aliyoyafanya yana msingi katika Shari´ah takasifu?

Jibu: Sunnah ni kutosoma kwa sauti ya juu katika swalah za kusoma kwa sauti ya juu. Ni sawa baadhi ya nyakati akisoma kwa sauti ya juu ili kuwatambuza waswaliji kwamba anaisoma na kwamba Basmalah ni kitu kimewekwa katika Shari´ah. Kwa sababu imethibiti kutoka kwa Mtume (Swalla Allaahu ´alyhi wa sallam) na makhaliyfah waongofu kutosoma kwa sauti ya juu.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Majmuu´-ul-Fataawaa (11/121)
  • Imechapishwa: 15/10/2021