Abu ‘Abdir-Rahmaan bin Hasan az-Zandiy al-Kurdiy amenitumia “Sa’qat-ul-Mansuur li Nasf Bid’ah wa Dhwalaalaat-ish-Shaykh Mashhuur”. Nilikipata kwa muda, lakini sikuweza kukisoma. Lakini baada ya watu wengi kuuliza kuhusiana na kitabu, hatimae ninakisoma hata hivyo nilikuwa nimebanika. Ni kitabu kizuri ambapo ndani yake amemradi Shaykh Mashhuur Hasan Aal Salmaan kwa mambo kadhaa. Baadhi yake ni haya yafuatayo:

1 – Amesema:

“Tunamthibitishia Allaah jicho bila ya kuweka mpaka, bi maana sio limoja wala mawili. Inatakiwa kuthibitisha bila ya kikomo kama ilivyotajwa. Yule mwenye kuwekea mpaka hilo alitolee dalili.”

Amefikishiwa maneno ya Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa sallam):

“Mola Wenu Hana jicho limoja tofauti na al-Masiyh ad-Dajjaal ambaye ana jicho limoja.”

Pamoja na hivyo amekataa na kubaki katika jambo lake.

2 – Anafanyia Takfiyr isiyokuwa ya moja kwa moja jamii ya Kiislamu.

3 – Anaruhusu uasi usiokuwa wa moja kwa moja kwa mtawala wa Kiislamu.

4 – Anaruhusu kujitoa muhanga jambo ambalo uharamu wake Ahl-us-Sunnah wamekubaliana nalo.

5 – Anatetea makundi ya uharibifu kama al-Ikhwaan al-Muslimuun na Jamaa´at-ut-Tabliygh.

6 – Anatetea, kuwapamba na kuwasifu Ahl-ul-Bid’ah. Kwa mfano, amesema kuhusu Jamaal-ud-Diyn al-Afghaaniy:

“Ni Mujaddid ambaye ametengeneza hali (Muswlih).”

Maneno hayo hayo amesema juu ya mwana-freemason Mmisri Muhammad ‘Abduh:

“Ni Mujaddid ambaye ametengeneza hali (Muswlih).”

Amesema kuhusu Sayyid Qutwub:

“Mwangaza wa mwanga.”

Amesema kuhusu al-Qaradhwaawiy:

“Mwanachuoni na msomi.”

Amesema kuhusu ´Adnaan Ar´uur:

“Wingu la elimu.”

Amesema kuhusu Abu Ghuddah al-Kawthariy:

“Mwanachuoni muhakiki na bingwa.”

Amesema kuhusu al-Maghraawiy Takfiyriy:

“Salafiy.”

Mlango wa mwisho wa kitabu unahusu Mashhuur Hasan kuwaponda kwake Ahl-us-Sunnah. Anawaponda kwa njia mbili:

1 – Kwa jumla. Miongoni mwa hayo amesema:

“Kama kuna wanachuoni, basi ni jambo lisilowezekana.”

Amesema pia:

“Wanachuoni hawako kwa ajili ya ´Awwaam.”

Wako kwa ajili ya nani kama sio kwa ajili ya ´Awwaam? Wanajibu maswali na wanafundisha. Wanaamrisha mema na kukataza maovu. Wanaita katika matendo mema na kutahadharisha maovu. Wanachuoni wanaeshi kwa ajili ya kufurahi na kukusanya pesa kwa njia ya halali na ya haramu? Wanaeshi kwa ajili ya kujisifu na kujitapa? Wanaeshi kwa ajili ya wao wenyewe kujisahihisha katika kumuabudu Allaah kwa matumaini na khofu. Wanaeshi kwa ajili ya watu kwa njia ya kuwafundisha na kuwanasihi na kuwabainishia haki kwa Da´wah na vitabu, hata kama watatofautiana [juu ya hilo].

2 – Makhsusi. Miongoni mwa mambo anayosema ni:

“Hasomi sana.”

“Ni mtu asiyejulikana.”

Mwandishi ameradi kila ambacho Mashhuur Hasan amechotaja na kubainisha haki na kuradi yalojificha. Kwa ajili hiyo ninapendelea vijana wasome Radd hii kutokana na faida ilionayo.

Ahmad bin Yahyaa an-Najmiy
1428/03/13

  • Mhusika: ´Allaamah Ahmad bin Yahyaa an-Najmiy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sa´qat-ul-Mansuur, uk. 8-10
  • Imechapishwa: 28/07/2020