Baadhi ya madhara yanayotokana na hasira

Imaam an-Nawawiy (Rahimahu Allaah) amesema:

16- Abu Hurayrah (Radhiya Allaahu ´anh) ameeleza kuwa kuna mtu alimuomba Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amuusie ambapo akamwambia: “Usighadhibike.” Yule mtu akakariri [kuomba kuusiwa] ambapo akamwambia tena: “Usighadhibike.”

Hakika ya hasira ni miongoni mwa sifa zenye kusemwa vibaya na ni miongoni mwa njia za Ibliys. hasira siku zote huambatana na shari. Mauaji mengi yanayotokea na magomvi huwa ni natija ya hasira. Kunatokea maneno mengi machafu, ambayo huenda mtu endapo angelitaka kujirudi angeweza kufanya hivo, lakini hatimaye anayatoa kwa sababu ya hasira. Matangamano mabaya mengi kati ya mtu na mke wake, talaka na mengineyo, chimbuko lake huwa ni hasira. Wanandugu kukatiana udugu mara nyingi na kutowaunga ndugu ambao Allaah (Jalla wa ´Alaa) Ameamrisha kuwaunga, sababu inayopelekea katika hilo huwa ni hasira. Hasira ni sifa yenye kusemwa vibaya na inatokana na shaytwaan. Hasira ni miongoni mwa njia za shaytwaan ambazo hutumia ili kuleta tofauti, mambo mabaya na ya haramu kati ya waumini wao kwa wao.

  • Mhusika: Shaykh Swaalih bin ´Abdil-´Aziyz Aalush-Shaykh
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh al-Arba´iyn an-Nawawiyyah, uk. 253-254
  • Imechapishwa: 14/05/2020