Baadhi wanaadhibiwa kwa mitihani, wengine wanapewa mitihani kwa kuwajaribu

Swali: Vipi tutaoanisha kati ya maneno ya Allaah (Ta´ala):

وَمَا أَصَابَكُم مِّن مُّصِيبَةٍ فَبِمَا كَسَبَتْ أَيْدِيكُمْ وَيَعْفُو عَن كَثِيرٍ

“Haukusibuni katika msiba wowote, basi ni kutokana ya yale yaliyochuma mikono yenu na anasamehe mengi.”[1]

na kati ya maneno yake (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam):

”Hakika Allaah anapowapenda watu basi huwapa mtihani.”?[2]

Jibu: Ndio, pindi Allaah anapowapenda watu basi huwapa mtihani. Ina maana kwamba wakati watu wanapokuwa wema na wakanyooka basi Allaah huwapenda na huwapa vilevile mtihani. Hakuna mgongano kati ya hayo mawili. Baadhi wanaweza kufikwa na mitihani kwa sababu ya madhambi yao na wengine wanaweza kupewa mitihani kwa ajili ya kuwajaribu.

[1] 42:30

[2] at-Tirmidhiy (2396), na Ibn Maajah (4031). Nzuri kwa mujibu wa al-Albaaniy katika ”Swahiyh-ul-Jaami´” (2110).

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Ighaathat-il-Lahfaan (84) http://alfawzan.af.org.sa/ar/node/17577
  • Imechapishwa: 28/12/2017