Kuwasaidia waislamu kwa hali yoyote

Swali: Je, ni wajibu kwetu kuwasaidi waislamu hata kama yaliyowafika ni kutokamana na madhambi yao?

Jibu: Ndio:

إِنَّمَا الْمُؤْمِنُونَ إِخْوَةٌ

“Hakika waumini ni ndugu.”[1]

Muislamu anatakiwa kumsaidia ndugu yake:

”Mfano wa waislamu ni kama jengo moja; upande mmoja unaupa nguvu upande mwingine.”[2]

”Mfano wa waislamu katika kupendana kwao, kuhurumiana kwao na kuwa na hisia ni kama kiwiliwili kimoja. Pindi kiungo kimoja kinapohisi maumivu, basi mwili mzima unapatwa na homa na kukosa usingizi.”[3]

Waumini ni ndugu. Wanafurahishwa na yale yenye kuwafurahisha ndugu zao na wanapatwa na uchungu kwa yale yanayowapa uchungu ndugu zao.

[1] 49:10

[2] al-Bukhaariy (2446) na Muslim (2585).

[3] Muslim (2586).

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Ighaathat-il-Lahfaan (84) http://alfawzan.af.org.sa/ar/node/17577
  • Imechapishwa: 28/12/2017