Baada ya kuswali amekumbuka amekula nyama ya ngamia

Swali: Mwenye kukumbuka baada ya swalah kuwa amekula nyama ya ngamia ni lazima arudi kuswali?

Jibu: Ndio, kwa kuwa wudhuu wake umetenguka kwa kula nyama ya ngamia. Aliulizwa (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) kama mtu anatakiwa kutawadha kwa kula nyama ya ngamia ambapo akajibu kwa kusema:

“Ndio.”

Akikumbuka kuwa ameswali na hakutawadha baada ya kula nyama ya ngamia anatakiwa kutawadha tena na kuirudi swalah yake.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Duruus-ul-Haram http://www.alfawzan.af.org.sa/node/13379
  • Imechapishwa: 24/06/2020