Baada ya kugombana mume hataki kumpa idhini ya kutoka

Swali: Kulitokea tofauti kati yangu mimi na mume wangu na yeye yuko katika safari. Ninapotaka kumuomba idhini ya kutoka nawasiliana naye kwa kumtumia meseji ya simu lakini hanijibu. Nikitoka bila ya idhini yake nakuwa ni mwenye kupata dhambi pamoja na kujua kuwa safari yake ni ndefu?

Jibu: Ndio. Usitoke isipokuwa kwa idhini yake. Haitoshelezi kwa kule wewe kumjulisha tu, ni lazima atoe idhini. Isipokuwa tu kama kuna haja ya kidharurah unayohitajia wakati yeye anakuwa hayupo na wewe huna yeyote anayeweza kukusaidia kwa hilo, katika hali hii utatoka kiasi cha haja. Utatoka kutekeleza haja unayohitajia pamoja na kujisitiri, heshima na kufupisha wakati kiasi na itakavyowezekana.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: http://www.alfawzan.af.org.sa/sites/default/files/al_makruf%204-13-08-1433.mp3
  • Imechapishwa: 16/06/2015