Swali: Mtu anatamka shahaadah na akachinja kwa jila la Allaah lakini haswali. Je, ni halali kula kichinjwa chake?
Jibu: Ikiwa anaacha swalah kwa makusudi, si halali kichinjwa chake kwa sababu ameritadi kutoka katika Uislamu:
”Ahadi iliopo kati yetu sisi na wao ni swalah. Hivyo basi, yule atakayeiacha amekufuru.”[1]
[1] at-Tirmidhiy (2621), an-Nasaa’iy (463) na Ibn Maajah (1079). Swahiyh kwa mujibu wa al-Albaaniy.
- Muhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
- Tarjama: Firqatunnajia.com
- Marejeo: Sharh ´Umdat-il-Fiqh (41)
- Imechapishwa: 19/10/2023