Swali: Ibn Mas´uud (Radhiya Allaahu ´anh) ameeleza kuwa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

“Yule katika nyinyi atakayeona maovu, basi ayakemee kwa mkono wake. Asipoweza, afanye hivo kwa ulimi wake. Asipoweza, basi afanye hivo kwa moyo wake – na hiyo ni imani dhaifu kabisa.”[1]

Jibu: Bi maana hana imani katika yale yanayohusiana na kuamrisha mema na kukataza maovu. Haina maana kuwa ni kafiri. Sio kafiri. Daraja ya mwisho ya ukemeaji ni kwa moyo. Hakuna kinachobakia baada ya kukemea kwa moyo.

[1] Ahmad (10766) na Muslim (49).

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/21985/معنى-حديث-ليس-وراء-ذلك-حبة-خردل
  • Imechapishwa: 16/10/2022